Monday, June 25, 2012

Police hold Dar bar owner over head in toilet



Kinondoni Regional Police Commander, Charles Kenyela
 
Police in Dar es Salaam have arrested the owner of Bongo Star Bar and Guest House James Isame (50) in Kawe on allegation of possessing a human head believed to be of a person with albinism.
Kinondoni Regional Police Commander Charles Kenyela said in an interview yesterday that the suspect was arrested in Kawe area on Saturday around 20:45 hours after an impeccable source tipped off the police.
“We are interrogating him at Kawe Police Station after finding him with a human head,” he said, adding: “We got the information from our sources…our officers surrounded him immediately…the head was found in his toilet”.
Kenyela said police were still interrogating Isame and information about him had been forwarded to the State Attorney’s Office for further actions.
Attacks on people with albinism have resulted in 78 deaths, hundreds permanently maimed and others psychologically devastated countrywide, particularly in Lake Zone regions of Kagera, Mwanza, Shinyanga and Mara.
Despite many arrests, there have been only 10 trials culminating in a mere 8 convictions, with most suspects left languishing in remand prison instead of being tried in court.
Recently a badly mutilated body of a person with albinism (PWA) was discovered at Nambala village in Kikwe ward, Arumeru district, a move which created fear and dismay among the community in Arusha region.
The body, which was discovered on May 26 2012 by children, was badly mutilated and left without clothes on a stone in the middle of River Nambala.
Attacks on people with albinism have been on the rise because the suspected ringleaders and witchdoctors are often not arrested and therefore don’t fear. Even more perplexing is the fact that people who pay for such horrors to be committed have never been identified in all the reported cases. 

Tuesday, June 19, 2012

DIAMOND KUMENYA USAFIRI MPYA

Msanii maarufu nchini kunako miondoko ya bongo fleva Diamond platnuzz amemenya usafiri mpya ikiwa ni kuendelea kuudhihilishia uma wa Watanzania kuwa kijana huyu anavuna mpunga mrefu kotokana na kipaji chake baada ya siku chache nyuma kutangaza kumiliki nyumba mbili za kifahali .


 

MSIMAMO WANGU WASASA JUU YA KAULIYANGU - JOHN MNYIKA


Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu
kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu
wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa
Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini
Mpango wa Taifa wa miaka mitano
kama Kiongozi Mkuu wa Nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri
Jeshi Mkuu. Na yeye ndiye Mwenyekiti
wa baraza la mawaziri, bajeti hii
iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa
imepita kwenye baraza alilloliongoza,
pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya
udhaifu wa taasisi ya Urais. Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye
ambaye anapeleka bajeti bungeni,
Waziri mwenye dhamana anapeleka tu
kwa niaba. Rais amepewa mamlaka
makubwa juu ya bajeti ibara ya 99
imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo
huku ibara ya 90 inasema bunge
likikataa bajeti rais ana mamlaka ya
kuvunja bunge. Hivyo Rais Kikwete
anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha
bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebisho!

Sunday, May 27, 2012

KANISA LA TAG ZANZABAR LACHOMWA MOTO KATIKA VURUGU ZILIZOTOKEA USIKU WA KUAMKIA JANA






 Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) liliopo mtaa wa Kariakoo mjini Unguja limechomwa moto jana usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana

POLOSI WAKITAWANYA WANDAMANAJI



Kikosi cha Kuzuwia Fujo FFU kikizunguka kikiwa kimejihami katika maeneo ya Michenzani ambapo tayari jeshi la polisi limepiga marufuku mikusanyiko yoyote Mjini hapa

WASIWASI mkubwa umetanda kwa siku ya pili mfululizo katika mitaa ya miji ya Zanzibar baada ya askari wa jeshi la polisi kupiga mabomu ya kutoa machozi ili kuwatawanya wafuasi wa taasisi za kidini zinaozongozwa na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI).

MANDAMANO ZNZ KUZUA TAAFULANI USIKU WA KUAMKIA JANA




Maelfu wa wazanzibari wakiongozwa na Taasisi za Kiislamu na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) wakifanya matembezi ya amani katika barabara za Zanzibar na kupeleka ujumbe wao kwa viongozi wa serikali za Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Umoja wa Mataifa wakitaka Zanzibar huru ambapo baadhi ya watembeaji hao wakiongoza na Kiongozi wa Jumuiya hizo, Sheikh Farid Hadi Ahmed na viongozi wengine
Maelfu ya wazanzibari leo wamefanya maandamano amani kuishindikiza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuitisha kura ya maoni juu ya Muungano na kupeleka ujumbe kwa Umoja wa Mataifa wa kutaka Zanzibar kujitenga kama ilivyofanya Sudan ya Kusini

Friday, May 18, 2012

Image of PICHA ZINGINE HAAHAHAH

Nilivyoona picha hii nilijiuliza hawa watoto walikuwa wanacheza mchezo gani ndipo mpiga picha wa kanjanja akawapiga hii picha?aliewapiga picha aliwatengeneza ili apate hii picha au?mmh hata sijui maana watoto nao hasa siku hizi wanampenda Ben 10 ndio balaa unawakuta wanacheza mmoja atajifanya Ben 10, spider man au mwanamieleka John sina.
Image of 50 CENT HOSPITALINI.
Rapper 50 Cent mwenye umri sawa na Afande Sele (Miaka 36) amelazwa hospitali huko Marekani ambapo mshkaji wake wa karibu Dj Drama amesema jamaa anasumbuliwa na tumbo “stomach virus” na sio ishu kubwa sana, bado mipango mingine iko palepale ikiwemo tarehe atakayoiachia mixtape yake mpya ya “The Lost Tape” May 22 mwaka huu.



ONA MASHABIKI NA WACHEZAJI WA SIMBA WANAVYOMLILIA MTESA MAFISANGO
Kiungo wa Simba, Patrick Mafisango ‘Mutesa’, amefariki jana alfajiri katika ajali ya gari iliyotokea katika barabara ya Chang’ombe maeneo ya Chuo cha Ufundi, Veta, jijini Dar es Salaam.
Mtandao huu uliushuhudia mwili wa marehemu ukiwa umetapakaa damu nzito ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mchezaji huyo alipata ajali hiyo akitokea Klabu ya New Maisha kuelekea nyumbani kwake ambapo ndani ya gari aliyokuwa akiendesha aina ya Toyota Cresta lenye namba za usajili T 387 BMZ kulikuwa na wenzake watatu ambao wote walitoka salama kwenye ajali hiyo




Uhuru Seleman wa Simba akilia kwa huzuni baada ya kufika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Kiungo wa Yanga na mchezaji wa timu ya taifa ya Rwanda, Haruna Niyonzima akiwa na majonzi kwa kifo cha mwenzake anayetokea Rwanda pia.

Rapper Jay Z amejitokeza hadharani na kuwa wa kwanza kuunga mkono kauli iliyotolewa na rais Barack Obama wa Marekani kuhusu kusupport ndoa za jinsia moja. Akiamplfy na CNN, Jigga amesema suala la kutoruhusu ndoa za jinsia moja kwa siku nyingi limekua likibagua uhuru wa watu.
Tamasha kubwa la caribbean beat ambalo linafanyika kesho katika viwanja vya posta ground -Kijitonyama jijini DSM maarumu kwa kumbukumbu ya mhasisi wa reggae hayati ROBART NESTA MARLEY aliyezaliwa mawakla 1945-1981ambapo kwa sasa ni miaka 31 tangu The great Jamaica's most beloved icons Boby Marley passed in a hospital in Miami after battling cancer.
Aliyekuwa Mshiriki wa Big Brother Stargame 2012, Julio Batalia akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mchana huu kuhusu ushiriki wake katika jumba lile la Big Brother

Wednesday, May 9, 2012

HAHAAHATARIIII

GARI LA MFANYABIASHARA MMOJA MKUBWA HAPA NCHINI AMBAYE ANAFANYA BIASHARA ZAKE  ZA NDIZI KUTOKA BUKOBA -DSM

Sunday, May 6, 2012

PYTHON VS CROCODILE

Angalia hapo wote wababe lakini mmoja anakosa msosi na kumezwa kizembe

Friday, May 4, 2012

NYARAKA ZA OSAMA BIN LADEN KUCHAPISHWA LEO

Marekani imechapisha baadhi ya nyaraka zilizokamatwa kwenye maficho ya mwisho ya aliyekuwa kiongozi wa mtandao wa al Qaida, Osama bin Laden. Nyaraka hizo zinaionyesha al Qaida kama kundi lililozingirwa na kudhoofika.
Nyaraka hizo ambazo ziliwekwa kwenye mtandao Alhamisi, ni sehemu ndogo tu ya zile zilizogunduliwa na Marekani, baada ya wanajeshi wake kumvamia na kumuuwa Osama bin Laden nchini Pakistan mwaka uliopita. Wamefanya makusudi, kuonyesha upande mbaya sana wa al Qaida, kwa sababu kuuawa kwa bin Laden kunachukuliwa na utawala wa Rais Barack Obama kama tukio muhimu kwa usalama wa taifa. Tukio hilo pia ni mada inayopendelewa sana na Rais Obama katika kampeni yake ya kutaka kuchaguliwa tena.

RAIS JAKAYA KIKWETE KUWAJIBISHA MAWAZIRI WALIOKIUKA UTENDAJI KAZI KATIKA WIZARA ZAO

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amewafuta kazi mawaziri waandamizi katika baraza lake la mawaziri. Katika mabadiliko hayo, waziri wa fedha Mustapha Mkullo ni miongoni mwa waliowekwa kando.
Mawaziri wapya waliochukua nafasi mpya kuwapisha walioachwa ni kama ifuatavyo (walioachwa majina kwenye mabano), Waziri wa Nishati na Madini - Profesa Sospeter Muhongo (William Ngeleja), Waziri wa Fedha - Dr William Mgimwa ( Mustapha Mkullo), Waziri wa Uchukuzi - Dr Harrison Mwakyembe (Omar Nundu), Waziri wa Maliasili na Utalii - Khamis Kagasheki (Ezekiel Maige), Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii - Dr Hussein Mwinyi (Dr Haji Mponda) na Waziri wa Viwanda na Biashara - Dr Abdallah Kigoda (Dr Cyril Chami).

PREZZO NDANI YA BBA

Ni superstar wa kimataifa kutoka nchini Kenya "PREZZO" akiwa katika pozi la nguvu tayari katika maandalizi ya shindano kubwa baarani Afrika yanayo julikana kama"Big Brother Africa" yanayotarajia kuanza mwishono mwa wiki hii nchini Afrika ya Kusini.

PUNGA

Ndo matatizo ya kuiga katika sayari ya kizazi cha sasa hivi kweli huyo ameona wanawake wanao vaa bikini wanafaidi sasa mpaka akaamua naye kujalibu au ndo pigo zake

Kanjanja

Hapa kanjanja sasa na glas zangu za kinafiki niko natega bingo ya ukanjanja siunajua tena bahasha nini afu ukijaulizwa stori inatoka lini aaaaaaaa kesho kwenye tttttv aaa gazzzzt aaa rediooooo banaaaa mhuuuuuu wananaona utamuuuuuuu

Thursday, April 26, 2012

wakali wa basketball kutoka NBA ndani ya studio za choice fm jijini DSM tayari kwa kukipiga na wabongo ikiwa wataanzia ROCK CITY,A CITY na kumalizia DSM

UNAIJUA HISTORIA YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR? HII HAPA


MKATABA, HATI NA MAMBO 11 YA MUUNGANO
Mkataba wa Muungano ulitiwa saini na Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964, Zanzibar.
     Ulithibitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi Aprili 26, 1964, na Aprili 27, 1964 viongozi hao walikutana katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Dalaam kubadilishana hati za Muungano.
    Sheria za Muungano ilitamka kwamba, Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zililazimika,  kuwa dola ya Jamhuri kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, jina ambalo lilibadilishwa Oktoba 28, 1964 na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia sheria ya Jamhuri ya Muungano, sheria namba 61, ya mwaka 1964.
     Msingi wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ni Hati za Muungano za Mwaka 1964.
     Hati za Muungano zilitiwa saini na Nyerere na Karume, Aprili 22, 1964 na hapo Tanganyika na Zanzibar kuwa dola moja kwa misngi inayotambulika kimataifa. Baada ya kuungana, Mwalimu Nyerere alikuwa rais wa kwanza na Karume alikuwa makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
      Aprili 26, 1964, bunge la Tanganyika lilipitisha sheria za Muungano, ambazo baadayezilithibitishwa na Baraza la Mapinduzi Zanzibar.
      Mnamo Aprili 27, 1964 waasisi wa Muungano walibadilishana Hati za Muungano na wajumbe saba wa Baraza la Mapinduzi waliapishwa kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Watanganyika na Zanzibar ambao ni Amani Karume, Kassim Abdallah Hanga, Abdulrahman Babu, Hassan Nassor Moyo, Aboud Jumbe, Hasnu Makame na Idris Abdul Wakil. Kati yao, Aboud Jumbe na Hassan Nassor Moyo wangali hai.
     Katiba ya muda ya mwaka 1965 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilianisha mambo 11 ambayo yalikubalika kuwa ni ya Muungano ambayo ni; Katiba na Serikali ya Muungano, Mambo ya nchi za nje, Ulinzi, Polisi, Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari, Uraia, Uhamiaji, Mikopo na Biashara za nje, Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa Tanzania unaosimamiwa na idara ya forodha, Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu.
      Katiba ya muda ya mwaka 1965 ilianisha utawala wa serikali ya mfumo wa chama kimoja, TANU kwa Bara na ASP kwa Zanzibar. Katiba hii, ilizingatia misingi ya makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 na sheria za Muungano wa Tangayika za Zanzibar.
      Katiba hiyo ilianisha serikali mbili, uwakilishi wa Zanzibar katika bunge la Muungano ikiwa na mamlaka juu ya mambo yote ya Muungano na mambo yasiyo ya Muungano kwa upande  wa Tanganyika. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwa na mamlaka juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano yahusuyo Zanzibar.
       Hata hivyo mambo ya Muungano yaliongezwa kutoka 11 hadi 22 kutokana na mahitaji ya ndani ya nchi pamoja na mabadiliko yaliyokuwa yanaendelea kutokea ulimwengini baada ya Muungano.
       Mwaka 1985, jambo la 12 linalohusu sarafu na fedha kwa ajili ya malipo na kurahisisha usimamizi wa fedha za kigeni na benki katika Jamhuri ya Muunagno wa Tanzania, liliingizwa.
     Kufuatia kuundwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1967, mambo matatu ya Muungano yaliyongezwa, ambayo ni leseni za viwanda na takwimu; elimu ya juu; na usafirishaji wa anga.
     Mwaka 1968, mambo ya maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya magari na ama ya petroli na aina nyingine za mafuta au bidhaa na gesi asilia yaliyongezwa kwenye orodha hiyo.
Aidha mambo ya Muungano yaliendelea kuongezeka hadi kufikia 21 kufuatia kuvunjika kwa iliyokuwa  Jumuiya ya Afrika Mashariki.
     Mwaka 1992 kufuatia mabadiliko ya mfumo wa siasa nchini suala la 22 la uandikishaji wa vyama vya siasa na mambo mengine yanayohusiana navyo liliongezwa kwenye orodha hiyo.
      MJADALA KUHUSU MUUNGANO
Katika miaka hivi karibuni kumekuwa na mijadala mbalimbali kuhusiana na muundo wa Muungano, baadhi wakitaka uwe wa zaidi ya serikali mbili, wengine serikali moja, wapo wanaotaka Tanganyika iwe kivyake na Zanzibar kivyake.
      Hata hivyo hekima inaonyesha kwamba Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unabaki kuwa ni fahari ya Watanzania, kwani mwelekeo wa dunia katika nyanja mbalimbali, mataifa kuungana kwa ushirikiano wa aina mbalimbali ni muhimu kuliko taifa moja kupambana kivyake.
      Urejeaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kuvunjika mwaka 1977, uwepo wa SADC, ECOWAS, COMESA, na jumuiya nyingine nyingi duniani kote, ni vielelezo kwamba ushirikiano baina ya mataifa ni suala lisilohitaji mjadala.
       Ieleweke kwamba hakuna ushirikiano usio kuwa na matatizo kama ilivyo kwa Muungano wa Tanzania, vivyo hivyo muungano mwingine kama vile ya United Kingdom (UK), Uingereza na United States of America (USA) kwa maana ya Marekani na United Arabs Emirate (UAE), nayo ina matatizo, lakini hata mara moja mjadala juu ya matatizo hayo siyo kuvunja ushirikiano bali kutatua na wale wanaotaka kuvunja hushughulikiwa ipasavyo.
      "Matatizo ya Muungano kama wa UK ni mabaya zaidi, na hata UAE hawana ahueni, ila wanajua kwamba Muungano wao ni lazima. Wamarekani wanapambana na watu wenye mawazo haya ya kuvunja miungano kwenye majimbo ya Alaska, Hawaii na Texas na mwishowe wameamua kuweka kambi kubwa ya jeshi la nchi kavu Texas; utitiri wa kambi za anga Alaska; na vituo vikubwa kupindukia vya majini kule Hawaii. Hivi, hawa mabingwa wa demokrasia wanapoamua kulinda nchi yao namna hii, unafikiri ni wajinga? Walimwaga damu na waliyanunua majimbo haya na wamepitia shida kubwa, ndiyo maana leo wanajidai," anaandika mchangiaji katika mjadala kuhusu Muungano.
        Ni vyema Watanzania wakati huu wa kusheherekea miaka 48 ya Muungano, kila mmoja akajisikia ufahari wa kuwa na kitu kizuri kilichoasisiwa na Waafrika wenyewe na kudumu kwa umri huo.         Mawazo ya kubaguana kwa sababu zisizo na msingi, pengine kukidhi matakwa na wakati kama vile ya kibinafsi na kisiasa, yasipewe nafasi kuisambaratisha nchi. Chambilecho wahenga, umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.

Wednesday, April 25, 2012

Bondia CHEKA ajifua kwa pambano kali la jumamos hii dhidi ya MAUGO

Kocha wa mchezo wa Masumbwi Abdalah Ilamba 'Komandoo' akimfanyisha mazoezi ya kukaza misuli ya tumbo bondia Francis Cheka Dar es salaam jana Chaka anajiandaa na mpambano wake na Mada Maugo utakaofanyika jumamosi hii katika ukumbi wa PTA Sabasaba ambapo mshindi atakuwa bingwa wa Mkanda wa I.B.F na atanyakua Zawadi ya gari.Picha na
kanjanja.
 

WASANII MABOROZI WAZURI WA MALARIA TANZANIA

Wasanii nchini kunako miondoko ya bongo fleva wameonekana kuleta mapinduzi makubwa katika kukabiliana na janga la ugonjwa wa maralia nchini,ikiwa wajikita zaidi katika uhamasishaji jamii sambamba na kubadilisha dhana ambazo zilikuwa zikijengeka jakatika jamii kuhusu matumizi ya vyamdarua.