Tuesday, June 19, 2012

MSIMAMO WANGU WASASA JUU YA KAULIYANGU - JOHN MNYIKA


Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu
kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu
wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa
Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini
Mpango wa Taifa wa miaka mitano
kama Kiongozi Mkuu wa Nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri
Jeshi Mkuu. Na yeye ndiye Mwenyekiti
wa baraza la mawaziri, bajeti hii
iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa
imepita kwenye baraza alilloliongoza,
pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya
udhaifu wa taasisi ya Urais. Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye
ambaye anapeleka bajeti bungeni,
Waziri mwenye dhamana anapeleka tu
kwa niaba. Rais amepewa mamlaka
makubwa juu ya bajeti ibara ya 99
imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo
huku ibara ya 90 inasema bunge
likikataa bajeti rais ana mamlaka ya
kuvunja bunge. Hivyo Rais Kikwete
anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha
bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebisho!

No comments:

Post a Comment