Friday, May 18, 2012




ONA MASHABIKI NA WACHEZAJI WA SIMBA WANAVYOMLILIA MTESA MAFISANGO
Kiungo wa Simba, Patrick Mafisango ‘Mutesa’, amefariki jana alfajiri katika ajali ya gari iliyotokea katika barabara ya Chang’ombe maeneo ya Chuo cha Ufundi, Veta, jijini Dar es Salaam.
Mtandao huu uliushuhudia mwili wa marehemu ukiwa umetapakaa damu nzito ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mchezaji huyo alipata ajali hiyo akitokea Klabu ya New Maisha kuelekea nyumbani kwake ambapo ndani ya gari aliyokuwa akiendesha aina ya Toyota Cresta lenye namba za usajili T 387 BMZ kulikuwa na wenzake watatu ambao wote walitoka salama kwenye ajali hiyo




Uhuru Seleman wa Simba akilia kwa huzuni baada ya kufika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Kiungo wa Yanga na mchezaji wa timu ya taifa ya Rwanda, Haruna Niyonzima akiwa na majonzi kwa kifo cha mwenzake anayetokea Rwanda pia.

No comments:

Post a Comment