Friday, May 4, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE KUWAJIBISHA MAWAZIRI WALIOKIUKA UTENDAJI KAZI KATIKA WIZARA ZAO

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amewafuta kazi mawaziri waandamizi katika baraza lake la mawaziri. Katika mabadiliko hayo, waziri wa fedha Mustapha Mkullo ni miongoni mwa waliowekwa kando.
Mawaziri wapya waliochukua nafasi mpya kuwapisha walioachwa ni kama ifuatavyo (walioachwa majina kwenye mabano), Waziri wa Nishati na Madini - Profesa Sospeter Muhongo (William Ngeleja), Waziri wa Fedha - Dr William Mgimwa ( Mustapha Mkullo), Waziri wa Uchukuzi - Dr Harrison Mwakyembe (Omar Nundu), Waziri wa Maliasili na Utalii - Khamis Kagasheki (Ezekiel Maige), Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii - Dr Hussein Mwinyi (Dr Haji Mponda) na Waziri wa Viwanda na Biashara - Dr Abdallah Kigoda (Dr Cyril Chami).

No comments:

Post a Comment